Posts

Showing posts from November, 2018

HEBU TURUDI SHULE KIDOGO,(NGUVU YA KUSHINDA).

Image
*HEBU TURUDI SHULE KIDOGO!* Biology inasema, baada ya tendo la ndoa mbegu za kiume zinazoingia kwa mwanamke ni takribani mbegu milioni mia tatu(300,000,000) na zote huanza kuogelea kuelekea kwenye ovum (yai). Kati ya hizo mbegu milioni 300 zinazofanikiwa kufika sehemu husika kwenye yai ni mbegu 500 tu, nyingine huchoka mapema na kufa njiani. Vilevile katika hizo mbegu 500 zilizofanikiwa kufika kwenye yai ni mbegu moja tu ndiyo hushinda na kuingia ndani kutengeneza kiumbe! *Mbegu hiyo ni wewe unayesoma ujumbe huu...* Biology inatuambia kuwa ulikimbia mbio na kuwashinda wenzio milioni 300 na ndiyo maana leo hii upo duniani... Usingekuwa mshindi katika mbio zile leo usingekuwepo duniani... *Je, umeshawahi kufikiri juu ya hili!?* Ulikimbia bila macho, mikono wala miguu na ukashinda! Ulikimbia bila elimu yako, ujuzi wala vyeti na ukashinda! Ulikimbia tena bila msaada wa mwingine yeyote na ukashinda... *Ni kitu gani leo cha kukufanya uwaze kushindwa katika maisha kiasi cha k

PENDO NDANI YA NDOA

Image
lv sura 10 kur. 110-120 Audio Player 26:02 SURA YA 10 Ndoa—Zawadi Kutoka kwa Mungu Mwenye Upendo “Kamba yenye nyuzi tatu haiwezi kukatika upesi.”— MHUBIRI 4:12 . 1, 2. (a) Nyakati nyingine tunajiuliza nini kuhusu wenzi wapya wa ndoa, na kwa nini? (b) Tutazungumzia maswali gani katika sura hii? JE, UNAPENDA kwenda kwenye arusi? Wengi wanapenda, kwa sababu mara nyingi hizo huwa pindi zenye kufurahisha sana. Bwana na bibi-arusi wanavalia mavazi yenye kupendeza kwelikweli. Zaidi ya hilo, nyuso zao zinaonyesha kwamba wana shangwe nyingi! Siku hiyo, wana furaha nyingi na inaonekana wana matazamio mengi mazuri ya wakati ujao. 2  Hata hivyo, ukweli ni kwamba ndoa nyingi leo ziko mashakani. Ingawa tunawatakia mema wenzi wapya wa ndoa, nyakati nyingine tunajiuliza: ‘Je, ndoa hii itakuwa na furaha? Itadumu?’ Majibu ya maswali hayo yanategemea ikiwa mume na mke wanaamini na kutumia shauri la Mungu kuhusu ndoa. ( Metha

MAJANI YA MPERA NA FAIDA ZAKE MWILINI.

Image
MAJANI YA MPERA NA FAIDA ZAKE MWILINI. 🍊 ---------------------- 1. Chai ya majani ya mpera inaponyesha kifua na kikohozi. 2. Majani ya mpera yaliyosagwa vizuri yanatumika kutibu muwasho uliotokana na mzio (allergy). 3. Pia majani haya ya mpera yakichemshwa kama chai yanaondoa cholesterol iliyozidi mwilini. 4. Chai ya majani ya mpera inapunguza kiwango cha tatizo la sukari mwilini. 5. Chai ya mpera ni dawa nzuri kwa wenye matatizo ya nguvu za kiume. 6. Pia inatumika kama scrub ya uso. Chukua majani ya mpera saga kisha tia maji kiasi na inasaidia kuondoa uchafu usoni. 7. Pia majani ya mpera yakichemshwa ni dawa ya kuponyesha tumbo la kuhara. 8. Kama umejikata kidogo unaweza kutumia majani ya mpera yalioshwa na kusagwa vizuri kwa kupunguza maumivu na kukulinda na maambukizi ya bakteria. 9. Majani ya mpera yaliyosagwa vizuri yanatumika kutibu eneo la mwili lililong'atwa na mdudu na kupunguza maumivu. 10. Chai ya majani ya mpera inaaminika kuwa ina uwezo wa kutibu tezi dum

FAHAMU UTAJIRI UPATIKANAO KWENYE KILIMO CHA KARANGA.

Image
Mogriculture Tz TOGGLE NAVIGATION Published by  Mtalula Mohamed  on  March 6, 2017  updated on  March 27, 2018 Kilimo Bora Cha Karanga Hutazikosa tena, weka email yako tukutumie makala zingine kama hii...     Subscribe Utangulizi Karanga ni mojawapo ya mazao yanayotoa mafuta. Katika Tanzania zao hili hustawi zaid katika mikoa ya Kusini Mashariki, Dodoma na Morogoro. Pamoja na kutoa mafuta vile vile zao hutumika kwa njia nyingine mbali mbali, nazo ni pamoja na: Chakula cha wanyama / mifugo (Mashudu na majani), kurutubisha ardhi na chakula cha binadamu: kutafuna na kuunga kwenye mboga/chakula (Confectionary) Kwa ujumla zao hili hutumika na wakulima kama zao la biashara. Hali ya Hewa Karanga hustawi vizuri katika maeneo yaliyopo kwenye miinuko chini ya mita 1500 toka usawa wa bahari katika Tanzania, na hustawi zaidi katika maeneo ambayo yanapata mvua za wastani wa mm 750 hadi mm 1200 kwa mwaka. Vile vile k