JINSI FENI INAVYOWEZA KUFANANISHWA NA ROHO, WA BWANA NDANI YA WOKOVU.



FENI.
kipepezi ama kifaa kinachotumia kupunguza kiwango cha joto mahala Fulani.
Leo mda mchache nlikuwa naitazama feni yangu Roho wa Bwana akanipa ufunuo huu.
Ya kuwa 
1.Feni haitengenezi joto.
2.Wala feni haitengenezi baridi.
Ni muundo wa mapanga ambayo wagunduzi waliyaunda yasukume upepo ukufikie.
Je! Ushawahi jiuliza kwa nini kuna wakati unatumia feni na bado unajisikia joto.
Wagunduzi waligundua kuwa katika mgandamizo wa hewa kuna some amount ya hewa baridi na ndio maana mara nyingi ukitumia feni inaleta ubaridi.(nadhalia)
Lakn nipo hapaaaa
Feni nikaifananisha na Roho mtakatifu kuwa usipowasha na kuielekezea kwako kamwe huwezi pata kaubaridi, 
Pia nikaifananisha na wokovu kuwa huwezi kuupata pasipo kuekezea kwako.
Ukiachana na hyo nikaifananisha na fursa ya kuwa usipoielekezea kwako kamwe huwezi kuipata .
Je unakumbuka kitabu cha Mwanzo sura ya 1 kabisa.
Mwanzo 1:1-3
[1]Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.
[2]Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.
[3]Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru.
Na unakumbuka Yesu alichokisema kwenye
Marko 8:34
[34]Akawaita mkutano pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, Mtu ye yote akitaka kunifuata na ajikane mwenyewe, ajitwike na msalaba wake, anifuate.
Aha na kumbe maisha ya Leo ni kama feni 
Ukitaka upepo wa baridi lazima uiwashe uilelekezee kwako nayo itakuburudisha
Na
Ndivyo ulivyo wokovu na neema ya kumfuata Kristo
Sasa Wokovu ndio ule upepo unakuja vizuri kabisa.
Feni ndiye Roho wa Mungu.
Na Umeme ndiye kristo mwenyewe.
unachotakiwa ni kuamua kuiwasha ile feni na mambo yote yafanye kazi kama yatakiwavyo.
Mbarikiwe kwa kuelewa.
Mwansasu'$

No automatic alt text available.

Comments

Popular posts from this blog

Picha ya kutisha ya Mtoto wa miezi nane kulawitiwa na baba yake mzazi.

MAJANI YA MPERA NA FAIDA ZAKE MWILINI.