Posts

Showing posts from February, 2017

Picha ya kutisha ya Mtoto wa miezi nane kulawitiwa na baba yake mzazi.

Image
INASIKITISHA :: Mtoto wa miezi nane abakwa na baba yake mzazi baada ya mama yake kuenda kazini. Mtoto huyu aliachwa na mfanyakazi Wa ndani , dada Wa kazi alienda sokoni na mtoto kumuacha kwa jirani. Baba Wa huyu mtoto karudi na nyumbani na kumkuta  Dada hayupo, ndipo alipoamua kuenda kumuulizia kwa jirani. Akakuta yupo mtoto, akamchkua mtoto na kuenda nae nyumbani. Baada ya hapo kilichotokea ni kumbaka mwanae.

TAZAMA AJARI MBAYA ILIYOTOKEA HIVI PUNDE...KIBONZO NA S.O.G

Image
Tumeshuhudia kupungua kwa ajiri nyingi naona zinataka kuanzia upya....nyuma ya mitaa baada ya kuri wawili kugongana baada ya uchovu mkali wa Siku.

KRC Genk Inayochezewa na Mbwana Samatta Inaungana na Man United 16 Bora ya Europa League

Image
Usiku wa February 23 2017 mtanzania Mbwana Samatta akiwa na timu yake ya KRC Genk ya Ubelgiji aliingia kwenye headlines baada ya kufanikiwa kufuzu kucheza hatua ya 16 bora ya Europa League kwa kuitoa FC Astra ya Romania. Samatta akiwa na KRC Genk waliikaribisha FC Astra ya Romania katika mchezo wao wa pili wa marudiano wa Europa League, katika uwanja wa Luminus Arena ikiwa ni wiki moja imepita toka watoke sare ya 2-2 ugenini. Katika game hiyo ya marudiano iliyochezwa na KRC Genk kupata ushindi wa goli 1-0 lililofungwa na Pozuelo kwa faulo dakika ya 67, wameiondoa FC Astra kwa jumla ya goli 3-2, hivyo Genk wanaungana na timu nyingine 15 kucheza hatua 16 bora ya Europa League ikiwemo Man United.

NAPE Atoa Mkwala Mkali Mechi ya Simba na Yanga...Adai Ukikasirika Nenda Kavunje TV Nyumbani.

Image
  February 23 2017 wakati wa uzinduzi wa mfuko wa kuchangia Serengeti Boys Waziri wa habari, Sanaa, utamaduni na michezo Nape Moses Nnauye amezungumzia kuhusu mashabiki wataokwenda kutazama mechi ya Simba na Yanga Jumamosi hii February 25 2017 uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Waziri Nape amewashauri tu mashabiki ambao hawawezi kuwa na uvumilivu pale matokeo ya mechi yanapokuwa mabaya kwa upande wao “Jumamosi kuna mechi ya Simba na Yanga mtakumbuka mechi iliyopita kulikuwa na matatizo lakini nawaomba watanzania tuweke ustaarabu na uzalendo wetu mbele” “Kama ukikasirika kunywa maji au nenda nyumbani, tunaomba tusiharibu miundombinu ya uwanja, Simba wanajua gharama waliyotumia kuukarabati uwanja ule, ukiona huna moyo wa kukaa uwanjani basi kaa nyumbani kwako angalia katika TV ukikasirika vunja TV yako” – Nape

HELA Wanazotuhumiwa Kupewa Kina TID Zilitolewa na Nani na Kutoka Fungu Gani?

Image
Clip iliyosambaa toka jana katika mitandaoni ya kijamii akisikika Mama Wema Sepetu na Steve Nyerere imezua Maswali mengi ikiwemo haya hapa chini: 1. Hiyo milioni mbili inayotajwa kuwa TID kapewa imetolewa na nani? 2 .Kama kweli baadhi ya walionekana kwenye vyombo vya habari watakuwa wamepewa hela, itakuwa wamepewa jumla ya shilingi ngapi? 3. Inawezekana mtu akatoa hela hizo zote kutoka mfukuoni mwake? 4. Kama kuna kikundi au taasisi ndio imehusika kutoa hizo fedha,watatoa tu hela zao hivi hivi bila kuwa na maslahi? 5. Kama kuna maslahi,yatakuwa ni maslahi gani? 6 .Kwasababu zoezi hili lilikuwa likiratibiwa na serikali,inawezekana kuna mkono wa serikali? 7 .Kama kuna mkono wa serikali,ni afisa gani kahusika na amezitoa katika fungu gani? 8 .Kama hizi "clip" ni fake,kuna yoyote miongoni mwa wanaotajwa amejitokeza kukana yanayosemwa? 9. Mama Sepetu na Steve Nyerere kuna yoyote kati yao amejitokeza kuzikana hizo clip mpaka sasa? 10. Kama hizi clip ni za kw

BREAKING News: Tetemeko la Ardhi Lenye Ukubwa wa 5.7 Latikisa Zambia na Tanzania

Image
    Tetemeko la ardhi ya ukubwa wa 5.7 kwenye vipimo vya Richter limekumba maeneo ya Ziwa Tanganyika mapema Ijumaa. Tetemeko hilo lilitikisa maeneo ya kaskazini mwa Zambia na mitetemeko hiyo ikasikika maeneo ya kusini magharibi mwa Tanzania. Kitovu cha tetemeko hilo, kwa mujibu wa Shirika la Utafiti wa Jiolojia la Marekani, kilikuwa kilomita 10 chini ya ardhi umbali wa kilomita 45 kutoka mji wa Kaputa nchini Zambia. Mji huo unapatikana katika mpaka wa nchi hiyo na Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Tetemeko hilo lilitokea mwendo wa saa tisa na dakika thelathini na mbili usiku (0032 GMT). Tetemeko la ardhi la ukubwa kama huo huchukuliwa kuwa la kadiri lakini wataalamu wanasema kutokana na hali kwamba kitovu chake chakikuwa chini sana ndani ya ardhi, huenda hilo lilisababisha mitikisiko kuwa mikubwa. Desemba mwaka 2005, tetemeko kubwa la ardhi lilitokea eneo la Ziwa Tanganyika. Tetemeko hilo la nguvu ya 6.8 lilitikisa majumba katika miji maeneo ya Afrika

WAZIRI Mahiga Abainisha Kisa cha Watanzania Kutimuliwa Msumbiji

Image
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Philip Mahiga amesema kuwa Watanzania waliokuwa nchini Msumbiji wamefukuzwa kutokana na kukiuka taratibu na sheria za kuishi nchini humo. Mahiga amesema kuwa Watanzania hao wamefukuzwa Msumbiji baada ya kubainika kuwa wanaishi nchini humo bila kuwa na pasipoti za kusafiria, vibali vya kuishi na kutofuata vigezo walivyokuwa wamepewa na mamlaka husika ya nchi hiyo. Hayo ameyasema wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ugeni unaotarajiwa kuwepo nchini Tanzania wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni anayetarajiwa kufanya ziara ya siku mbili ya Kitaifa nchini Februari 25 na 26, 2017. Rais wa Visiwa va Shelisheli, Mhe. Dannu Faure naye atawasili Tanzania kwa ziara ya siku mbili kuanzia Tarehe 27-28, februari mwaka huu.

MZEE wa Upako Amuonya Nay wa Mitego Baada ya Kudai Anakuja na Kanisa lake

Image
Baada ya hivi karibuni msanii wa hip hop, Nay wa Mitego kutangaza kuwa atafungua kanisa lake ambalo litakuwa si la biashara bali ni la kumuabudu Mungu aliye hai, Mchungaji maarufu nchini, , Lusekelo Anthony aka Mzee wa Upako amemuonya kutomchezea Mungu. Mzee wa upako ameyasema hayo alipotafutwa na E-News ya EATV baada ya kuulizwa maswali juu ya kauli hiyo. “Kama unakuja kanisani kwa maana kuna biashara, nakupa miaka hii mitatu sio utatembelea ndala utatembelea kucha, ni mtoto mdogo sana hana akili. Mungu hataniwi, anafanya kufuru, kama ana mama yake amemzaa amuonye. Mimi biblia nimesoma na hizo lugha zake nyepesi zitamtokea puani, asithubutu kufanya kanisa kama biashara. Baada ya miaka hii mitatu atajua kwamba kuongoza watu sio kama kuongoza ngo’mbe hakuna jambo gumu kama kuongoza watu wenye akili kama wewe wenye ufahamu kama wewe, wapo watu wengi walianzisha makanisa kwanini walifunga, ujinga hujui ni ujinga ni utoto,” Alisema Mzee wa Upako.

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Chaipinga TCU, Chasema Hakijawahi Dahili Wanafunzi Vilaza

Image
Siku moja baada ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kutangaza utata wa udahili wa wanafunzi wa vyuo vikuu, wadau wakubwa wa elimu, wamejitokeza kupinga hatua hiyo. Wadau hao ni pamoja na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) . UDSM kimeeleza kwamba hakuna mwanafunzi hata mmoja aliyedahiliwa chuoni hapo, ambaye hana sifa za kujiunga na chuo hicho. Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Florens Luoga alisema jana kuwa chuo hicho kimeweka utaratibu ambao unaweza mwanafunzi yeyote anayedahiliwa chuoni hapo, awe na sifa zinazohitajika kwa kuwa hawafanyi biashara. “Sisi hapa ni wakali kuhusu jambo hilo, tukibaini kuwepo kwa mwanafunzi ambaye hana sifa tunamfukuza. Hatusubiri TCU iseme...hata tukibaini kuwa mtu alifanya udanganyifu na alishamaliza chuo, lakini hakuwa na sifa, tunamnyang’anya digrii tuliyompa,” alisema Profesa Luoga na kuongeza: “Hiki ni chuo, hatufanyi biashara, sisi kazi yetu hapa ni kuandaa wataalamu na ndio maana tunakuwa wakali na makini kuhakikisha

TIMU ya Leicester Wamtimua Kocha Wake...Kisa Kizima Hichi Hapa

Image
  Ranieri alikuwa Kocha wa Leicester tangu Julai 2015 Bingwa mtetezi wa ligi kuu England Leicester City imemtimua Kocha wake muitaliano Claudio Ranieri, ikiwa ni miezi tisa baada ya kuiwezesha kupata ubingwa wa Ligi kuu. Leicester iko katika nafasi ya 17, na ikipoteza alama moja tu itakuwa kwenye mstari wa kushuka daraja. Kutimuliwa kwa kocha huyo kumekuja saa 24 baada ya kichapo cha magoli 2-1 walichopata kutoka kwa FC Seville. Leicester City msimu uliopita ilitwaa ubingwa kwa zaidi ya alama 10 mbele, lakini msimu huu, mpaka sasa wamecheza michezo 25 ya ligi na kushinda mitano pekee, na imesalia michezo 13 ligi kuisha.

HII Ndiyo DNA ya Kitamaduni Kabisa Yenye Ukweli 90% Kujua Kama Mtoto ni Wako Au Umebambikiziwa

Image
Hapo nyuma nilikuwa nikiambiwa kuwa Wazee ni dawa na hazina hasa katika kutupatia Maarifa sisi Vijana na Wajukuu zao nilikuwa sitaki kuamini na kuna wakati hata nilikuwa nikimwona tu Mtu Mzee au Bibi basi nawapuuza tu nikiamini kwamba hawana jipya tena. Hali hii ilibadilika taratibu baada ya kuanza sasa kupenda kukaa na Wazee mara kwa mara ili niweze kuchota hekima na busara zao na kwa kweli tokea nianze kurudisha imani yangu kwa Wazee naona nimefaidika mno katika kupata Elimu dunia ambayo wengi wetu hatuna na tumebaki tu kujikita katika Elimu zetu hizi za Kitaaluma tukidhani kuwa pekee ndizo zitatukomboa Kifikra. Pamewahi kuwa na nadharia kwamba akina Babu na Bibi wao huweza kujua Mtoto mchanga aliyezaliwa leo kama ni Mjukuu wao kweli au labda Mtoto wao amebambikiwa huyo Mtoto na Mama yake kutokana na usaliti wake ndani ya Mahusiano yao. Niliamua kufanya mazugumzo yangu ya Kiudadisi kabisa na Wazee wa Mikoa mbalimbali ili tu niweze kujua kama kuna njia yoyote mbadal

DONALD Trump Atangaza Kujenga Kinu Kikubwa Cha Silaha za Nyuklia Marekan

Image
      Rais wa Marekani, Donald Trump ametangaza kuwa anataka kujenga kinu kikubwa cha nyuklia nchini humo kuhakikisha kuwa taifa hilo lenye nguvu zaidi duniani linaendelea kuwa juu zaidi katika silaha za nyuklia. Akizungumza leo katika mahojiano maalum na shirika la habari la Reuters, Rais Trump amesema kuwa Marekani sasa hivi iko nyuma katika uwezo wake wa silaha za atomiki. Katika hatua nyingine, Reuters imemnukuu Trump akizungumza baada ya mahojiano hayo, ambapo alieleza kuwa anachukizwa sana na kitendo cha Korea Kaskazini kufanya majaribio ya silaha zake za maangamizi. Alisema kuwa katika kuidhibiti Korea Kaskazini, Marekani inapaswa kutumia mfumo wa nchi marafiki kama Japani na Korea Kusini.

Ndivyo Mbowe Alivyofanikiwa Kuwatoroka Polisi Mchana Kweupe Wakati Wakimtafuta..!!!

Image
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam, limemtaka Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kujisalimisha Polisi mara moja kwa ajili ya Mahojiano yanayohusu vita vya dawa za kulevya baada ya juhudi za kumsaka katika makazi yake kushindikana huku simu yake ya mkononi ikiwa imezimwa  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Simon Sirro amesema Bw. Mbowe aliahidi kwenda mwenyewe juzi tarehe 15, lakini hakwenda lakini jeshi la hilo lilimtafuta usiku na mchana katika makazi yake na kumpigia simu lakini simu yake ilizimwa  Aidha jeshi hilo limesema watuhumiwa watatu Agnes Masogange, Rashid Idd au Chid Mapenzi na Wallis Latif Nasher ambaye ni muuza magari katika eneo la mikocheni watapandishwa kizimbani Jumatatu kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya lakini pia walibainika wanaotumia dawa hizo baada ya kupelekwa kwa Mkemia Mkuu  Katika kupambana na Askari feki, jeshi limemtia mbaroni aliyekuwa askari

Baada ya Wafanyakazi wa Manji Kukamatwa,Ubalozi wa India Waibuka na Tamko Hili Zito kwa Serikali ya JPM..!!!

Image
SIKU chache baada ya Idara ya Uhamiaji kukamata raia wa India kwa madai ya kufanya kazi bila vibali, Balozi wa India nchini, Sandeep Arya, ameingilia kati suala hilo na kusema tatizo lilikuwa mawasiliano kati ya mwajiri na Uhamiaji. Akizungumza jana , Balozi Arya alisema anaendelea kufuatilia kwa karibu suala hilo na kudokeza kuwa jitihada za kumaliza sintofahamu hiyo, zinaendelea kwa njia ya mazungumzo kati ya mwajiri na Idara hiyo. Akifafanua baada kumaliza kikao chake na wawakilishi wa kampuni 30 za kutengeneza dawa kutoka India zinazojiandaa kuwekeza nchini, Balozi Arya alisema baada ya kubaini tatizo kuwa mkanganyiko wa mawasiliano, ndiyo maana wameruhusu kampuni hizo kuwekeza nchini. “Unajua zipo ajira za muda, zingine miaka miwili, hivyo udhaifu wa mawasiliano ulisababisha sintofahamu, hivyo taratibu za kufanya ukaguzi zinapaswa kuchukuliwa na vibali vitolewe maisha yaendelee,” alisema. Balozi Arya alisisitiza kuwa jitihada za kumaliza sintofahamu hiyo

Dr Harrison Mwakyembe Aonywa na Chama cha Wanasheria Afrika Mashariki

Image
Chama cha Wanasheria Afrika Mashariki (EALS) kimemwandikia barua Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Harrison Mwakyembe kikimtaka aache kuingilia uchaguzi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS). Barua hiyo imekuja baada ya Dkt. Mwakyembe kudaiwa hivi karibuni kutishia kuifuta TLS kwa madai kwamba imeanza kuingiliwa kisiasa. Barua hiyo iliyoandikwa na kusainiwa na Rais wa EALS, Richard Mugisha, inasema TLS si chama cha kisiasa na kimeanzishwa kwa kufuata sheria zote. “Mheshimiwa Waziri, tumesikitishwa na taarifa ambazo zimeenea kwenye vyombo vyote vya habari na gazeti la East African la Februari 18 ambalo limekunukuu ukisema kwamba Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) kina muingiliano wa kisiasa,” inasema sehemu ya barua hiyo. Katika barua hiyo, Mugisha anasema wanasheria wanatakiwa wapewe uhuru, wasiingiliwe na serikali kama ilivyo kwa nchi nyingine kwani kuingilia ni sawa na kuvunja sheria za nchi. Rais wa sasa wa TLS, John Seka amesema kuwa chama chake kimefur

Wema Afunguka Sababu ya Kukimbilia CHADEMA

Image
Akizungumza na waandishi wa habari akiwa ameambata na mama yake mzazi nyumbani kwao Sinza Jijini Dar es Salaam, Wema amesema sababu kubwa ya kuhamia CHADEMA ni ili kupata nafasi ya kupigania demokrasia anayodai kuwa inapotea nchini Tanzania Tanzania. Sababu nyingine aliyoieleza Wema ni kutelekezwa na CCM licha ya kujitolea kutoa mchango wake kwa chama hicho wakati wa kampeni cha uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kiasi cha kuwa hatarini kumwagiwa tindikali visiwani Zanzibar. "Kuanzia sasa mimi siyo tena mwanachama wa CCM, na muda mfupi ujao nitachukua kadi yangu ya CHADEMA... Nimeamua kuingia CHADEMA kwa sababu nataka kupigania demokrasia, laiti ningejua, ningeingia zamani sana, najua nimewahi kusema kuwa nitakufa nikiwa CCM, lakini sikujua kama itakuwa hivi, laiti ningejua mapema basi nisingesema vile na ningejiunga CHADEMA muda mrefu sana". Amesema Wema Sepetu  Amesisitiza kuwa hajaamia CHADEMA kwa sababu ya pesa kama ambavo imekuwa ikidaiwa, bali ni kwa ajili y

TCRA Yaadhibu Vituo Vinne vya Utangazaji

Image
Dar es Salaam. Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)  imetoa adhabu kali kwa vituo vinne vya utangazaji  kwa kukiuka maadili ya utangazaji kwa mujibu wa sheria na kuvitaka viombe radhi siku tatu mfululizo kuanzia leo (Ijumaa) kupitia taarifa ya habari. Akitoa adhabu hizo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA, Valerie Msoka amesema vitio hivyo vimepewa onyo kali ikiwa ni pamoja na kutozwa faini na kuomba radhi wasikilizaji wake. Amevitaja vituo  hivyo kuwa ni Star TV,Channel ten, Clouds FM na Times FM.

KIBONZO CHA LEO NA S.O.G

Image
Kutojali usalama  Kuchapa     Barua pepe 0 Comments Muuza maji akiwa amedandia basi lililo kwenye mwendo bila ya kujali usalama wake, Barabara ya Nyerere, eneo la Vingunguti, Dar es Salaam.

JE, TUKIWASHUGHULIKIA WATUMIAJI WA MADAWA YA KULEVYA TUWAACHE MAJAMBAZI PATA HABARI HAPA.

Mihadarati sawa; tusiwasahau majambazi, matapeli viwanja IMECHAPISHWA: 22 FEBRUARI 2017  Kuchapa     Barua pepe 0 Comments “SISI tumekwisha uwasha Mwenge na kuuweka juu ya Mlima Kilimanjaro, umulike hata nje ya mipaka yetu ulete tumaini pale ambapo hapana matumaini, upendo penye chuki na heshima ambapo pamejaa dharau.” Maudhui ya wimbo huu ulioimbwa siku Tanzania ilipouwasha Mwenge wa Uhuru na kuuweka juu ya Mlima Kilimanjaro yameanza kuonekana katika Tanzania mpya tnayoiona sasa. Serikali “imewasha mwenge” wa vita dhidi ya dawa za kulevya kwa wazalishaji, wasafirishaji, wauzaji na watumiaji. Vita hii inahitaji nguvu ya pamoja kwa kuwa madhara ya dawa za kulevya yanawakumba wana jamii wote kiuchumi, kijamii na kiafya. Hii iwe vita ya wote. Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli inaonekana kuthubutu kuutafuna mfupa uliowashinda wengi. Rais Magufuli ameridhia, amebariki na kuagiza vita ianze na kuendelea bila mwisho. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul

NAPE AWAPA SHAVU WATENGENEZA N WAUZAJI WA FILAMU TANZANIA.

Image
Nape afafanua uingizwaji filamu za nje IMEANDIKWA NA  GRACE MKOJERA IMECHAPISHWA: 22 FEBRUARI 2017  Kuchapa     Barua pepe 0 Comments SERIKALI imesema haina matatizo na filamu za kutoka nje kama zitafuata sheria na utaratibu wa nchi. Akizungumza jana na wasanii wa filamu kuhusu namna ya kuboresha sera ya filamu, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye alisema sheria zilizopo hazibagui filamu za ndani wala za nje zote zinahitaji kufuata utaratibu wa bodi ya filamu. “Hatuwezi kugeuza nchi yetu kuwa kisiwa kwamba filamu zisiingie kabisa hapa haiwezekani, ugomvi wa serikali tunazo sheria ambazo kwa sasa ndio zinasimamia utaratibu wa kuingiza na kuuza filamu kutoka nje,” alisema. “Najua yapo maneno kwamba masharti ya uingizaji wa filamu kutoka nje ni magumu na wanasema hayatekelezeki lakini kwa kuwa sheria ipo, lazima ifuatwe… kama mtu atafuata utaratibu hata kama atausa sh bilioni 10 hatapata matatizo,” alisema. Waziri Nape pia ametangaza kuw

ONGEZEKO LA WATUMIAJI WA MITANDAO YA KIJAMII LAONGEZEA TANZANIA.

Image
Watanzania mil. 16 wanatumia mitandao ya intaneti IMEANDIKWA NA  NASHON KENNEDY, MWANZA IMECHAPISHWA: 22 FEBRUARI 2017  Kuchapa     Barua pepe 0 Comments IMEELEZWA kuwa karibu nusu ya wakazi wa dunia wanatumia mitandao, wakati nchini Watanzania milioni 16 wanafanya shughuli zao kwenye mitandao mbalimbali ya intaneti. Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Dk Hassan Abbas, ameyasema hayo wakati anazindua tovuti mpya 37 za mikoa mitano na Halmashauri 37 nchini zitakazokuwa zikitumiwa na maofisa habari na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) katika hafla iliyofanyika jijini hapa. Amesema kutokana na hali hiyo, watu wengi kwa sasa wanatumia muda wao mwingi wakisoma nyaraka, matukio na vitu mbalimbali kuliko hata kusoma magazeti. Amewataka maofisa habari hao kuzitumia tovuti hizo vizuri kwa madai kuwa ni nyenzo muhimu itakayowawezesha kutekeleza majukumu yao kwa wakati na zaidi kutoa taarifa sahihi za maendeleo kwa wananchi na kwa wakati. "Tumieni

MADIWANI WASUSA DODOMA

Image
Madiwani Dodoma hawamtaki Meya, wasusa IMEANDIKWA NA  MAGNUS MAHENGE, DODOMA IMECHAPISHWA: 22 FEBRUARI 2017  Kuchapa     Barua pepe 0 Comments BAADHI ya madiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamegoma kuendelea na kikao cha chama kilichokuwa kikiendeshwa na mwenyekiti wao, Meya wa Manispaa ya Dodoma, Jafari Mwanyemba kwa kumtuhumu kwa ubadhirifu wa fedha. Madiwani hao walitoka nje ya ukumbi wa mkutano, baada ya Meya Mwanyemba kukataa kumpisha katibu wa madiwani aongoze kikao. Madiwani hao wanamtuhumu Mwanyemba kwa ubadhirifu wa Sh milioni 30 za mradi wa maji wa Zuzu. Akizungumza na kwa niaba ya madiwani 47 wa chama, Naibu Meya wa Manispaa hiyo, Jumanne Ngede alisema mradi huo wa maji ulilenga kuuwanufaisha wakazi wa kata ya Zuzu, lakini utekelezaji wake umekuwa ukisuasua kutokana na kugubikwa na ubadhirifu wa fedha za mradi huo. Ngede ambaye ni diwani wa Chamwino alisema kutokana na tuhuma hizo kumkabili Meya Mwanyemba, madiwani 43 kati ya 47 wa chama, wal

HUWEZI AMINI UKIUFAHAMU UKWELI KUHUSU MADAWA YA KULEVYA DUNIANI

Tatizo la madawa ya kulevya limetokea kuwa janga kubwa duniani kote, watu wengi wameathirika na janga hili. jinsia zote wanaume, wanawake, na vilevile rika zote vijana na wazee pia. Hapa tutaongelea aina mbili za madawa ya kulevya yaani Cocaine na Heroin. Cocaine Hutokana na majani ya mmea uitwao kitaalamu Erythroxylum coca bush. Aina hii ya dawa ya kulevya hutolewa kwa mifumo ifuatayo; Unga ambapo mitaani hujulikana kama ‘coke’ na hutumika kwa kuvutwa puani kama unga, au kuyeyushwa na maji na kuchomwa kwenye mshipa wa damu. Crack ambapo mitaani hujulikana kwa jina hilohilo crack au rock, na hutengenezwa kwa kuchanganywa na kemikali. Na hutumika kwa kuvutwa kama sigara. Cocaine pindi inapoingia kwenye damu huenda kwenye ubongo na kuzuia ufyonzwaji wa vihisishi vifuatavyo: dopamine, norepinephrine na serotonin, kutoka kwenye ubongo. Hivyo ubakia kwenye ubongo. Na vihisishi hivi husababisha ile hali ya furaha, mchangamfu na kujisikia mwenye nguvu kitaalamu eup

MJUE RAISI MUGABE KAMA RAISI ANAYEONGOZA KWA UMRI MKUBWA DUNIANI

Image
Alizaliwa mnamo mwaka 1924 pia aliwahi kufungwa jela mwaka 1964 na kutoka mwaka 1974 kwa kosa la kutoa hotuba ya kuihujumu Serikali. Lakini pia Umoja wa Ulaya(EU) umemuongezea muda wa vikwazo Mugabe, yeye pamoja na Mkewe Grace kwa mwaka 1 hadi tarehe 20 Februari mwakani. Hata hivyo Rais Mugabe amesema kuwa Donald Trump hakuwa chaguo lake upande urais wa Marekani lakini pia hakupenda Bi. Clinton ashinde kwakuwa angekuja kusimamia na kuviendeleza vikwazo iliyopewa nchi ya Zimbabwe.

Habari za mjin

Tunapatikana hapa