NAPE AWAPA SHAVU WATENGENEZA N WAUZAJI WA FILAMU TANZANIA.

Nape afafanua uingizwaji filamu za nje

SERIKALI imesema haina matatizo na filamu za kutoka nje kama zitafuata sheria na utaratibu wa nchi. Akizungumza jana na wasanii wa filamu kuhusu namna ya kuboresha sera ya filamu, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye alisema sheria zilizopo hazibagui filamu za ndani wala za nje zote zinahitaji kufuata utaratibu wa bodi ya filamu.
“Hatuwezi kugeuza nchi yetu kuwa kisiwa kwamba filamu zisiingie kabisa hapa haiwezekani, ugomvi wa serikali tunazo sheria ambazo kwa sasa ndio zinasimamia utaratibu wa kuingiza na kuuza filamu kutoka nje,” alisema.
“Najua yapo maneno kwamba masharti ya uingizaji wa filamu kutoka nje ni magumu na wanasema hayatekelezeki lakini kwa kuwa sheria ipo, lazima ifuatwe… kama mtu atafuata utaratibu hata kama atausa sh bilioni 10 hatapata matatizo,” alisema.
Waziri Nape pia ametangaza kuwafutia leseni wauzaji wa filamu feki waliokamatwa hivi karibuni katika operesheni iliyofanyika Kariakoo ili waombe upya kwa kuzingatia taratibu za nchi.
Alisema katika operesheni hiyo aligundua uuzwaji wa filamu nyingine zisizokuwa na maadili kama za ushoga ambazo kama zikitazamwa na vijana basi maisha yao yatakuwa hatarini.
Alisema sheria iliyopo ya mwaka 76 itaendelea kutumika hadi itakapotengenezwa sera na sheria nyingine itakayoendana na mabadiliko ya kibiashara na kuwanufaisha wasanii.
Katibu wa bodi ya Filamu, Joyce Fisso alizungumzia baadhi ya changamoto zilizotolewa na wadau ikiwemo sekta hiyo kutokuendeshwa kwa mtizamo wa kibiashara, upungufu katika mfumo wa kisera na kisheria lakini pia sekta hiyo kuendeshwa kwa mfumo usio rasmi.
Alisema uandaaji wa sera mpya utasaidia kuondokana na changamoto zilizopo na kusaidia sekta hiyo kufikia malengo yake. Baadhi ya wasanii walitoa maoni yao na miongoni mwao ni Herman Mnenule ‘Master Shivo’ ambaye aliomba serikali kuweka sheria ngumu dhidi ya wanaosambaza kazi feki na kutoa adhabu ya kifungo.
Aidha, Single Mtambalike ‘Rich’ alisema sanaa inatakiwa ifanywe kama biashara na sio burudani.
Alisema wasanii wanabanwa na utamaduni kwani wanashindwa kushindana na filamu za nje.
“Kwa mfano, kuna lugha tukizitumia tunaambiwa sio tamaduni za nchi, wenzetu wanapewa magereza, nguo za polisi na kuigiza sera za nchi zao lakini sisi tunaedit sana, tunaomba sera mpya ituangalie na kutusaidia,” alisema.
Hata hivyo, wasanii, wasambazaji, wapigapicha, watayarishaji , waongozaji waliomba kufanyike kikao kwa kila kundi ili kutoa maoni kwa uhuru.
Wiki ijayo watayarishaji watakutana na bodi ya filamu na Wizara hiyo lengo ni kutoa maoni yao juu ya uboreshwaji wa sera.

Comments

Popular posts from this blog

Picha ya kutisha ya Mtoto wa miezi nane kulawitiwa na baba yake mzazi.

MAJANI YA MPERA NA FAIDA ZAKE MWILINI.