Baada ya Wafanyakazi wa Manji Kukamatwa,Ubalozi wa India Waibuka na Tamko Hili Zito kwa Serikali ya JPM..!!!

SIKU chache baada ya Idara ya Uhamiaji kukamata raia wa India kwa madai ya kufanya kazi bila vibali, Balozi wa India nchini, Sandeep Arya, ameingilia kati suala hilo na kusema tatizo lilikuwa mawasiliano kati ya mwajiri na Uhamiaji.
Akizungumza jana , Balozi Arya alisema anaendelea kufuatilia kwa karibu suala hilo na kudokeza kuwa jitihada za kumaliza sintofahamu hiyo, zinaendelea kwa njia ya mazungumzo kati ya mwajiri na Idara hiyo.
Akifafanua baada kumaliza kikao chake na wawakilishi wa kampuni 30 za kutengeneza dawa kutoka India zinazojiandaa kuwekeza nchini, Balozi Arya alisema baada ya kubaini tatizo kuwa mkanganyiko wa mawasiliano, ndiyo maana wameruhusu kampuni hizo kuwekeza nchini.
“Unajua zipo ajira za muda, zingine miaka miwili, hivyo udhaifu wa mawasiliano ulisababisha sintofahamu, hivyo taratibu za kufanya ukaguzi zinapaswa kuchukuliwa na vibali vitolewe maisha yaendelee,” alisema.
Balozi Arya alisisitiza kuwa jitihada za kumaliza sintofahamu hiyo, zinaendelea kwa njia ya mazungumzo na ofisi yake kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania, watahakikisha suala hilo linamalizika kidiplomasia bila kuathiri ushirikiano uliopo

Comments

Popular posts from this blog

Picha ya kutisha ya Mtoto wa miezi nane kulawitiwa na baba yake mzazi.

MAJANI YA MPERA NA FAIDA ZAKE MWILINI.