NAPE Atoa Mkwala Mkali Mechi ya Simba na Yanga...Adai Ukikasirika Nenda Kavunje TV Nyumbani.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiMatwbsIkN_RAVjiNYkJ_6Hf_Fo7dtCmGyKQ5z6J9wL3TOfPzg9z2Ldb4zy_b_n6_7LN7zdCoIC4AeE5FsaRLvR3GCzsWKdDaoR6D84ZEjSD4d2DwasNLsPR78_rtlHy_WK4Oj_8b7ywWV/s2560/%25255BUNSET%25255D.jpg 

February 23 2017 wakati wa uzinduzi wa mfuko wa kuchangia Serengeti Boys Waziri wa habari, Sanaa, utamaduni na michezo Nape Moses Nnauye amezungumzia kuhusu mashabiki wataokwenda kutazama mechi ya Simba na Yanga Jumamosi hii February 25 2017 uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Waziri Nape amewashauri tu mashabiki ambao hawawezi kuwa na uvumilivu pale matokeo ya mechi yanapokuwa mabaya kwa upande wao “Jumamosi kuna mechi ya Simba na Yanga mtakumbuka mechi iliyopita kulikuwa na matatizo lakini nawaomba watanzania tuweke ustaarabu na uzalendo wetu mbele”

“Kama ukikasirika kunywa maji au nenda nyumbani, tunaomba tusiharibu miundombinu ya uwanja, Simba wanajua gharama waliyotumia kuukarabati uwanja ule, ukiona huna moyo wa kukaa uwanjani basi kaa nyumbani kwako angalia katika TV ukikasirika vunja TV yako” – Nape

Comments

Popular posts from this blog

JE !!!! UNAJUA HISTORIA SAHIHI YA WIMBO WA TAIFA LA TANZANIA NA MTUNZI WAKE NA NI NCHI GANI WANAIMBA TUNE SAWA NA WIMBO HUU.

Picha ya kutisha ya Mtoto wa miezi nane kulawitiwa na baba yake mzazi.

UFAHAMU UGONJWA WA MSHIPA WA NGIRI (HERNIA/HYDROCELE)