KIFAHAMU CHAKULA CHA KUZUIA KUZEEKA HARAKA
Maisha ya sasa hivi yamegubikwa na matumizi ya vipodozi vya kuzuia uzee hadi kufikia kiwango cha kuonekana kama ni chakula kuliko vitu vya urembo. Vipodozi hivyo huja kama creams, visafisha ngozi au serums. Lakini ieleweke kuwa kutumia vipodozi vya kuondoa uzee juu ya ngozi hakuwezi kuwa mbadala wa chakula ambacho kinaboresha mwonekano na kutunza ngozi yako kuanzia ndani. Chakula cha kuzuia kuzeeka haraka ndiyo kitu muhimu katika kuufanya mwili wako usizeeke haraka na katika kuulinda mwili wako kutokana na mionzi ya UV (ultra violet) ambayo ndio chanzo kikuu cha mistari na mikunyanzi juu ya ngozi yako. Ungana nami leo kuona ni chakula gani kinasaidia kutunza mwonekano wako wa ujana. Lakini kwanza tuvichambue vitu muhimu katika chakula vyenye uwezo wa kulinda mwili wako usizeeke haraka. Vitu Muhimu Katika Chakula Vya Kuzuia Kuzeeka Haraka Katika mada yetu ya Ondoa Uzee tuliona kwamba mahitaji ya mwili hubadilika kadr...