UGONJWA WA MSHIPA WA NGIRI (HERNIA/HYDROCELE) Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikilia au kubeba viungo fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiliwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo. Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji. Ugonjwa huu wa ngiri unawapata wanaume na wanawake wa rika zote. Mshipa wa ngili ni jina linalokusanya magonjwa kama Ngiri kavu (Hernia), Ngiri maji (Hydrocele) na Ngiri nyinginezo kama vile kuvimba kokwa au mfereji unaopitisha manii unaojulikana kitaalamu kama Epididmorchitis. Ngiri Kavu (Hernia), aina hii ya ngiri huwapata wanawake na wanaume wote kwa ujumla. Ngiri kavu inapompata Mwanamke huitwa Fermoral Hernia, na pindi inapompata mwanaume inaitwa Scro...
Comments
Post a Comment