Mama Janeth Magufuli, Tuna Mengi ya Kujifunza Kwake Kama Mama na First Lady. Mapito Yake ni Somo...!!!
Moja ya wanawake ninaowaheshimu sana hapa Tanzania akiwepo mama
yangu,mke wangu na wengineo ni mama Janeth Magufuli. nimekuwa kwa karibu
sana nikimfuatilia mama huyu na kugundua ni mwanamke wa kipekee hasa
ambaye katika miaka takribani 30 hajatokea First Lady wa aina yake nchi
Tanzania. ni mwanamke ambaye ana moyo ulioshiba kujiamini na wenye
umaskini wa majivuno.
huyu mama amekuwa akisimamia anachoamini na mara nyingi ameonekana akiwa
katika picha au video mbalimbali akionesha alicho nacho moyoni ni
kikubwa kuliko kile tunachokiona. ni mama ambaye aliridhika ana
ameridhika na kazi yake ya ualimu pamoja na kuwa mumewe alikuwa waziri
serikali iliyopita na hata sasa bado anaonekana kutamani kuendelea na
kazi yake ya ualimu ingawa inakuwa ni ngumu kutokana na mazingira ya
nafasi ya mumewe kwa sasa.
mama huyu ambaye amekuwa makini sana kusikiliza kila linalosemwa juu ya
mumewe ambaye ni rais wa nchi na kulipokea kwa hisia nzito sana
akihusisha na hali halisi ya maisha ambayo wamekuwa wakiishi na mumewe.
na hii imemfanya kuwa mama wa karibu na ambaye aliamua ku msupport
mumewe agombee urais katika mazingira magumu sana kisiasa nchi tanzania.
mama janeth alikubali ku msupport mumewe na kuzunguka naye nchi nzima
akimfanyia kampeni akionesha ustaarabu wa hali ya juu sana. mama huyu si
mwingi wa maneno... mara nyingi amekuwa mkimya na unaweza msoma vizuri
kupiia sura yake ya upole na yenye utulivu.
naamini huyu atakuwa mmoja ya first lady ambao hawatajilimbikizia mali
kupitia miradi na mifuko mbalimbali kama ilivyotokea huko nyuma. tuzidi
kumwombea Mungu amtie nguvu na ninaamini kwa namna ambavyo amepitia
mengi mpaka kufika hapo alipo tuna mengi ya kujifunza toka kwake.
na mwisho tumpongeze mh rais kwa kuweza kupata mke kama mama janeth
magufuli naamini analielewa hili kwa upana kabisa kuwa amepata mwanamke
ambaye ni wa aina yake katika siasa za tanzania. mwenye msimamo imara
lakini pia mwenye busara na kuamini anachoamini siku zote.
Comments
Post a Comment